Monday, January 30, 2017

MWENYEKITI WA CCM WILAYA APIGWA RISASI MGONGONI

mbeya-2MBEYA: 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29. 01. 2017 majira ya saa 05. 45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwele, Tarafa ya Ntebela, wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya.
Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala Kitandani nyumbani kwake Ntebela, ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za goroli.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa, Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda Lukula, amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kumuua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya ndugu Lobe Zongo akimpokea Mwaitenda katika hospitali ya rufaa Mbeya wakati alipofikishwa hospitalini hapo CCM wilaya ya Mbeya mjini ndugu Ephrahim Mwaitenda akifikishwa hospitalini hapo.
Source.
GLOBAL PUBLISHER.

0 comments:

Post a Comment