Monday, January 30, 2017

MHUBIRI ALIYEKUWA NA WAKE 86 NA WATOTO 203 AFARIKI DUNIA

Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa
Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.
Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake.
Wengine wao walikuwa wajawazito.
BBC iliripoti mwaka 2008 kuwa alikuwa na takriban watoto 170 lakini gazeti hilo lilisema kuwa aliwaacha watoto 203.
                                                             

0 comments:

Post a Comment