Wednesday, September 27, 2017

DULLY KAZI FT BLAST MUSIC,BLACK-----------FIKIRI KWANZA

Tuesday, January 31, 2017

TRUMP AMFUTA KAZI KAIMU MWANASHERIA MKUU WA MAREKANI.

                                                 
Rais wa Marekani, Donald Trump amemfuta kazi Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Sally Yates saa chache baada ya  kiongozi huyo kuwaagiza Mawakili kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo vya kuingia Marekani raia wa nchi saba zenye waislamu wengi.

Sally Yates aliyeteuliwa na Rais Obama alisema kuwa alitoa agizo hilo kwa Mawakili sababu haamini kama zuio la raia kuingia Marekani ni halali.

Rais Trump Ijumaa alitia saini amri inayozuia raia kutoka Somali, Sudan, Libya, Yemen, Iran, Syria na Iraq kuingia nchini Marekani ambapo zuio hilo ni la siku 90.

Maandamano yamezuka maneneo mbalimbali ya Marekani huku wakipinga zuio hilo. Wanadiplomasia wamesema kuwa zuio hilo huenda likasababisha hatari zaidi kwa usalama wa Marekani.

 Aidha, baadhi wamehoji kwanini zuio limewekwa kwa nchi hizo saba wakati kwa miaka ya hivi karibuni hakuna raia wake aliyehusika na ugaidi nchini Marekani?

Rais Trump amevikosoa vyombo vya habari vinavyopotosha kuwa  zuio hilo ni kwa Waislamu pekee. Rais Trump amesisitiza kuwa zuio hilo ni kwa raia wote wanaotoka katika nchi hizo hata kama si Waislamu.

Trump alisaini amri hiyo katika kile alichosema kuwa ni kuzuia watu wenye misimamo mikali kuingia nchini Marekani ikiwa ni hatua za kuimarisha ulinzi na usalama.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.


Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam

Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali

Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara 

Monday, January 30, 2017

NENO: KAMA ULIKOSA MAHUBILI YA EV.JACOB MBONILE HAYA HAPA

Kama ulikosa mahubili ya asubuhi ya mhubili Jacob Mbonile bonyeza hapa chini kusikiliza na ubarikiwe zaidi

HATIMAYE MOROCCO YARUDI KATIKA UMOJA WA AFRIKA AU.


Umoja wa Afrika umeamua kuirudisha Morocco katika shirika la Umoja wa Afrika AU zaidi ya miongo mitatu baada ya taifa hilo la ufalme wa Afrika Kaskazini kujiondoa katika AU kufuatia mgogoro wa eneo la Sahara magharibi.
Shirika hilo linatambui Sahara ya Magharibi kuwa jimbo huru, lakini Morrocco inasema kuwa eneo hilo ni mkoa wake wa kusini.
Morocco imepigania mpango wake wa kutaka kujiunga tena na Umoja wa Afrika mwaka uliopita.
Eneo la Sahara ya Magharibi linaendelea kuwa eneo tata ,lakini viongozi wengi wa Afrika walipiga kura kuikubali Morrocco kurudi katika Umoja wa Afrika.

MAREKANI: OBAMA ATOA YA MOYONI

                                                             
Ofisi ya rais wa zamani wa Marekani Barack Obama imetoa tamko na kusema kwamba raisi huyo wa zamani anakerwa na na maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga tamko la raisi Donald Trump kutaka kuweka vizuizi vya uhamiaji juu ya wasafiri kutoka kwa baadhi nchi za Kiislamu.
Msemaji wa raisi Barack Obama, Kevin Lewis, amesema kwamba raisi mstaafu Kimsingi hakukubaliana na wazo la ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya dini yao. Na kuongeza kusema kwamba wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kusikilizwa na viongozi waliochaguliwa na ndiyo matarajio yao pindi waonapo Marekani inaingia hatarini hatarini.

VIDEO:MFUNGWA AFAULU MTIHANI AKIWA GEREZANI

                                                  

Inatokea kwenye gereza la Naivasha Kenya ambapo Mfungwa Michael Kahiga ni miongoni mwa Wafungwa wachache watakaojiunga na chuo kikuu kutokana na jitihada zake za kujisomea kwa bidii chini ya Mwalimu wake pia ambaye pia ni Mfungwa wa kifungo cha maisha.
Kwenye gereza hilo la Naivasha kuna Liblary ambayo ina vitabu mbalimbali ambapo Michael anasema pamoja na yeye kufaulu kwenda chuo kikuu, kwenye kusoma kwake akiwa gerezani bado hakuwa na Waalimu ambao wamekidhi vigezo.
Michael anatumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya wizi ambapo baada ya kumaliza kifungo chake, atajiunga na chuo kikuu cha London Uingereza ambacho kimempa nafasi ya kusoma bure kwenye chuo hicho baada ya kufaulu vizuri kwenye mtihani wa kitaifa gerezani.
Kwa mujibu wa K 24 Kenya, kwenye mtihani aliofaulu Michael ni Wanafunzi 141 walipata A ambapo Michael mwenyewe alipata C+.
zaidi tazama video hii...